Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo leo Jumatano katika kikao na baraza lake la mawaziri ambapo amesisitiza kwamba, Iran inataka amani, uthabiti na usalama ulimwenguni sambamba na kuweko ushirikiano mzuri na mataifa yote ambayo yamechagua njia ya ushirikiano mzuri.
Dakta Hassan Rouhani ameongeza kuwa, Iran haijafurahi kwa namna yoyote ile kuingia madarakani nchini Marekani Joe Biden, hata hivyo imefurahi kuona kiongozi mbabe na mkiukaji mkubwa wa sheria katika nchi hiyo ameondolewa madarakani.
Aidha amesema, inasikitisha kuona kwamba, baadhi ya vyombo vya habari vya ndani vinaathirika na propaganda za vyombo vya habari vilivyo dhidi ya Iran kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kutofautisha mazingira ya sasa na ya mwaka 2015 kabla ya kufikiwa makubaliano hayo na kueleza kwamba, bila shaka mazingira ya leo ya Iran na ya wakati huo yanatofautiana.
Aidha amesema kuwa, mwaka 2015 fikra za waliowengi ulimwenguni zilikuwa zikiona kwamba, kama Iran itaahidi basi haitotekeleza ahadi yake, lakini kupitia makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa pamoja wa Utekelezaji JCPOA imethibitika kwamba, Iran ni nchi yenye kutekeza ahadi zaidi ulimwenguni na hushawishika kwa shida kwa ajili kufanya mazungumzo, lakini inapotia saini makubaliano fulani huwa ni yenye kuheshimu na kurekeleza kikamilifu makubaliano hayo.
342/